Tanzania Kukosa Misaada Ya Ulaya

JE, MMEYASIKIA YA BUNGE LA ULAYA.

Bunge la Ulaya limetoa uamuzi mzito unaobeba ujumbe wa kisiasa wa hali ya juu dhidi ya mwelekeo wa utawala wa sasa nchini Tanzania. Kupitia Kamati ya Mambo ya Nje (EP_ForeignAf) na Kamati ya Maendeleo (EP_Development), wabunge wa EU wamepiga kura kuzuia hatua ya Tume ya Ulaya kutoa fedha nyingi kwa Tanzania mwaka ujao kupitia mfuko wa NDICI–Global Europe – mfuko muhimu kwa kukuza maendeleo, ustawi na uwajibikaji barani Afrika.

Katika kura hiyo, wabunge 53 waliunga mkono kusitisha fedha hizo, huku 2 wakipinga na 1 akijizuia kupiga kura. Hii si kura ya kawaida. Ni tamko rasmi la kisiasa la kuonyesha kutoridhishwa na hali ya kisiasa, uchaguzi, na mwenendo wa haki za binadamu nchini.

READ Also  Robert Alai Reveals What Edwin Sifuna Will Do After Being Removed As SG

Kwa nini wamechukua uamuzi huu?

Sababu zao ni tatu kuu:

  1. Kukithiri kwa ukandamizaji wa wananchi – ikiwemo kubanwa kwa haki ya kujieleza, kuandamana na kukusanyika.
  2. Uchaguzi wenye utata na udanganyifu – kutokuwepo kwa uwazi, haki na uwanja sawa wa kisiasa.
  3. Mwelekeo wa kiimla wa Serikali – kuongezeka kwa matendo yanayoashiria kupotea kwa misingi ya demokrasia.

Kwa lugha nyepesi, Bunge la Ulaya limesema:

β€œHatutoendelea kutoa fedha kubwa kwa Tanzania huku demokrasia ikiendelea kupungua na wananchi wakizidi kunyanyaswa.”

Hii ina maana gani kwa Tanzania?

  1. Fedha za maendeleo Zinaweza kuzuia au kucheleweshwa hadi maboresho ya kisiasa yaonekane.
  2. Sifa ya Tanzania kimataifa Inaendelea kuharibika kutokana na tuhuma za ukandamizaji.
  3. Mahusiano ya Tanzania na EU Yanapitia mtihani mkubwa na presha itaongezeka.
  4. Serikali ya Tanzania Itahitaji kuchukua hatua kurejesha imani ya dunia
READ Also  Bad Day For Omanyala As He Finishes 5th In Tokyo

Uamuzi huu unakuja katika kipindi ambacho macho ya dunia yote yapo Tanzania. EU imeonyesha wazi kuwa haitatoa fedha za kujenga barabara na miradi ya maendeleo kwa taifa linaloshutumiwa kubomoa misingi ya haki, uhuru na demokrasia.

Onyo au Fursa?

Serikali inaweza kuchagua:

  1. Ama kuendelea na njia ya sasa na kupoteza washirika muhimu,
  2. Au kuanza kufungua mfumo wa kisiasa na kurejesha matumaini ya wananchi na jumuiya ya kimataifa.

Lakini jambo moja liko wazi:

πŸ‘‰πŸ½ Dunia imeamka. Na sasa inaangalia Tanzania kwa makini zaidi kuliko hapo awali.

Wasalaam
John Pambalu

  • Related Posts

    Football Titbits Across The Papers

    Paris St-Germain have no plans to pursue a move for Manchester City’s World Cup-winning Spain midfielder Rodri. (Sky Sports), external However, City are bracing themselves for a bid from Spanish…

    Football Titbits across the papers

    Real Madrid are working on a deal to sign Manchester City midfielder Rodri, with the Spanish club confident an agreement can be reached for the 30-year-old Spain captain. (Athletic –…

    You Missed

    Football Titbits Across The Papers

    • By Milton
    • July 28, 2026
    • 2 views
    Football Titbits Across The Papers

    Football Titbits across the papers

    • By Milton
    • July 25, 2026
    • 4 views
    Football Titbits across the papers

    𝗕π—₯π—˜π—”π—žπ—œπ—‘π—š: Cruise Missiles Hit Two Oil Tankers Near UAE

    • By Milton
    • July 14, 2026
    • 15 views
    𝗕π—₯π—˜π—”π—žπ—œπ—‘π—š: Cruise Missiles Hit Two Oil Tankers Near UAE

    𝗕π—₯π—˜π—”π—žπ—œπ—‘π—š: Europe Unites to Boost Air Defense Against Russian Missiles

    • By Milton
    • July 14, 2026
    • 11 views
    𝗕π—₯π—˜π—”π—žπ—œπ—‘π—š: Europe Unites to Boost Air Defense Against Russian Missiles

    Update: President Ruto Mourns

    • By Milton
    • July 14, 2026
    • 7 views
    Update: President Ruto Mourns

    Maseno University, Set To Admit A Record 9,196 Students

    • By Milton
    • July 9, 2026
    • 9 views
    Maseno University, Set To Admit A Record 9,196 Students