Habari ya Kutisha
Mtoto aliyepelekwa kunyolewa nywele ya kwanza kwa kina babaye ameuliwa kwa kukatwa shingo na ndugu wa baba kule Matioli- Butali, katika Kaunti ya Kakamega.
Inaarifiwa kwamba kijana huyo, Amondo Mola mwenye umri wa miaka 19, alimuua mtoto wa miezi minne kwa kumkata shingo kwa upanga.
Inasemekana mtoto huyo alikuwa amepelekwa nyumbani kwa familia ya kijana huyo kwa sherehe za kitamaduni za kunyolewa nywele.
Mama wa mtoto alikuwa amekubaliana na wazazi wa mwanaume aliyezaa naye kwamba ampeleke mtoto anyolewe nywele ya kwanza na nyanya.
Hata hivyo, alipowasili nyumbani hakuwapata wazazi. Badala yake alimkuta kijana huyo ambaye alimpokea mtoto, akaenda naye nyuma ya nyumba kisha kufanya mauaji hayo.
Polisi wamemkamata mtuhumiwa huku uchunguzi ukiendelea.
Tukio hili limeibua majonzi makubwa pale Matioli-Butali katika eneo la Malava.






