Mambo muhimu ya kuzingatia katika kuchagua aina ya kuku wa kufuga kibiashara ambapo kwa ufupi ni lazima uzingatie uwezo wa kupambana na magonjwa, kasi ya ukuaji, soko, utagaji wa mayai (mkubwa), gharama za matunzo, uzito na wingi wa nyama. Ufugaji wa kuku kibiashara umejikita katika aina kuu nne za kuku ambazo ni kuku chotara, kuku wa kienyeji (pure), kuku wa nyama (broiler) na kuku wa kisasa wa mayai (wasiohitaji jogoo).
Nitaenda kuelezea kwa kifupi breed / aina mbalimbali za kuku pamoja na sifa zake.
1 KUKU CHOTARA
Hii ni aina ya kuku ambao wanapatikana baada ya kuchanganya aina / breed mbili tofauti za kuku ili kupata breed moja ambayo inakua na sifa za pande zote mbili mfano jogoo wa broiler anaweza akachanganywa na mtetea wa kienyeji ambapo breed itakakayopatikana inakuwa na sifa za pande zote yaani upande wa baba (jogoo wa kisasa) na za upande wa mama (mtetea wa kienyeji).
Lengo la kutengeneza breed hii ya chotara ni kupata aina ya kuku ambao ni wastahimilivu sana wa magonjwa, wanaoweza kuishi katika mazingira tofauti, watagaji wazuri wa mayai, walaji wa chakula kidogo, wenye soko kubwa, miili mizito na mikubwa na wasio na gharama kubwa ya kuwatunza.
Zifutazo ni aina mbalimbali za kuku chotara ambao wanafugwa nchini Tanzania.
i. KUROILER
Hii ni aina ya kuku chotara ambao asili yake ni nchini India na ilianza kutengenezwa miaka ya tisini na mtaalamu aitwae Vinod kutoka Kegg Farms Private Ltd.
Breed hii imetokana na kuchanganya (crossing) kwa jogoo wa broiler (Sasso) au jogoo aitwae White Leghorn na mtetea aitwae Rhode Island Red. Jogoo hawa wana sifa ya kuwa na miili mikubwa na mtetea aina ya Rhode Island Red wana sifa ya kutaga mayai mengi. Kwa hiyo breed inayopatikana ambayo ni kuroiler inakuwa na sifa za pande zote mbili yaani wanakua na miili mikubwa ambayo wanarithi kutoka kwa baba zao (jogoo) na wanataga mayai mengi ambapo hii wanarithi kutoka kwa mama zao (mitetea) Kwa hiyo kuku hawa wanafaa kwa nyama na mayai.
SIFA ZA KUKU AINA YA KUROILER
Wanakua haraka (wamerithi kwa baba yaani jogoo)
Wanataga mayai mengi (wamerithi kwa mama yaani mtetea) ambapo endapo wakilishwa vizuri kwa mwaka wanaweza kutaga mayai 200-250 na huanza kutaga wakiwa na umri wa miezi mitano na nusu mpaka sita.wakati wa kienyeji pyua hutaga mayai 40-50 kwa mwaka.
Wanakua na uzito mkubwa hivyo wanafaa kwa nyama ambapo jogoo hufikisha kilogram 3.5 mpaka 5 ndani ya miezi mitano tu. Mtetea hufikisha kilogram 3 mpaka 3.7 wakati kuku wengine wa kienyeji wanafikisha kilogram 3 baada ya mwaka mmoja.
Nyama yao ni tamu na mayai yake ni mazuri kwa afya ya binadamu kwani yana kiini cha njano
Wanashahimili sana magonjwa (ingawa chanjo ni lazima uwapatie)
Gharama za kuwatunza ni ndogo
Wana uwezo wa kutaga mayai kwa muda wa miaka mitatu ila hawalalii mayai yao hivyo kama unataka kutotolesha vifaranga unatakiwa uwe na mashine ya incubator (ambayo utaipata kutoka kwetu) au uweke mayai kwa kuku wengine wanaolalia mayai.
Kwa hiyo kuku aina ya kuroiler ni wazuri sana kuwafuga kibiashara kutokana na sifa nilizozianisha hapo juu na aina hii ya kuku ni miongoni mwa breed inayofugwa na watu wengi sana hapa nchini.
ii. BLACK AUSTRALORP (KUKU WA MALAWI)
Hii ni aina ya kuku chotara ambao kwa muonekano wao wa nje wana manyoya ya rangi nyeusi iliyokolea. Sifa kubwa ya kuku hawa ni uwezo wao wa kutaga mayai mengi kwa muda mrefu. Kuku hawa wanataga mayai mengi zaidi ya kuroiler.Endapo ukiwalisha vizuri wana uwezo wa kutaga mayai 250 – 300 kwa mwaka mmoja. Huanza kutaga mayai wakiwa na umri wa miezi mitano na nusu. Pia wana sifa ya kuwa na miili mikubwa. Kama ilivyo kwa kuroiler, kuku hawa wanastahimili sana magonjwa (ingawa lazima uwapatie chanjo) na wanafaa kwa ajili ya mayai na nyama.
Kwa hiyo kuku aina ya Black Australorp (kuku wa Malawi) pia ni wazuri sana kuwafuga kibiashara.
iii. SASSO (COLOURED BREED)
Hii ni aina ya kuku chotara ambao asili yake ni nchini Ufaransa na pia wanajulikana kwa jina la coloured breed. Breed hii ilianza kutengenezwa na kampuni ya kifaransa iitwayo SASSO mwaka 1978. Kwa ufupi tunaweza kusema sasso ni kama vile broiler wa kienyeji kwani anakua haraka mfano endapo akipewa lishe bora, ndani ya miezi mitatu mpaka minne anakuwa tayari kwa kuuzwa hivyo kwa mwaka mmoja unaweza kufuga kwa vipindi vitatu tofauti yaani unanunua vifaranga mwezi wa kwanza halafu mwezi wa nne unawauza, ukishauza hao unanunua vifaranga wengine ambao baada ya miezi mine yaani mwezi wa nane unawauza na ukishauza unanunua vifaranga wengine ambao ndani ya miezi minne nao utawauza. Ufugaji wa kuku aina ya sasso utakusaidia kupata fedha nyingi ndani ya muda mfupi.
Sasso anaanza kutaga akiwa na umri wa miezi mitano ambapo kwa mwaka anaweza kutaga mayai zaidi ya 240 endapo akitunzwa vizuri.
iv. KENBRO
Hii ni aina ya kuku chotara ambayo ilianza kutengenezwa na kampuni ya kifaransa iitwayo Kenchic na kuzalishwa nchini Kenya. Kenbro wana rangi ya brown na ni kwa ajili ya matumizi ya nyama na mayai. Wana maumbo makubwa hasa jogoo ambapo hufikisha kilogram 4. Wanaanza kutaga wakiwa na miezi mitano na endapo wakitunzwa vizuri wana uwezo wa kutaga mayai zaidi ya 150 kwa mwaka ila hawaatamii mayai hivyo kama ukitaka kutotolesha lazima uwe na mashine ya incubator au uweke mayai kwa kuku wengine ambao wanaatamia mayai ingawa ukitumia mashine ndio bora zaidi.Hawa pia wanastahimili sana magonjwa ingawa lazima uwapatie chanjo na gharama za matunzo ni ndogo.
v. NEW HAMPSHIRE REDS (KUKU WA ISRAEL)
Hii ni aina yakuku chotara ambao wakitunzwa vizuri kwa mwaka wanaweza kutaga mayai 250 na kuendelea. Hukua haraka (jogoo hufikisha uzito wa kg 4 na mtetea kg 3 na huanza kutaga wakiwa na umri wa miezi mitano. Kama ilivyo kwa chotara wengine hawa pia wanastahimili sana magonjwa ingawa pia chanjo ni lazima uwapatie, gharama za matunzo ni ndogo , wanaweza kuishi katika mazingira tofauti pia wanakula chakula kidogo.
- KUKU WA MAYAI (LAYERS)
Hii ni aina ya kuku wa kisasa ambao ni spesho kwa ajili ya kutaga mayai. Yaani wanalishwa vizuri, wanapewa chanjo halafu wanataga mayai kwa wingi sana bila kupandwa na jogoo. Mayai yake hauwezi kutotoleshea vifaranga kwa kuwa hayana mbegu ya jogoo.Uzalishaji wa kuku hawa hufanywa na makampuni makubwa ya uzalishaji na uuzaji wa vifaranga ambao wanakua na kuku wazazi (parent stock) ambao hawapatikani hapa Tanzania kwa maana ya kwamba wanawanunua nje halafu wao wanakuwa wanawatumia kuzalishia kuku hawa wa kisasa wa mayai. Najua unaweza ukawa unajiuliza kwamba je mtetea wa kisasa akipandwa na jogoo wa kienyeji mayai yatakayopatikana yanaweza kutumika kutotoleshea vifaranga? Jibu ni ndio inawezekana lakini vifaranga watakaopatikana watakuwa hawana ubora unaotakiwa na utakua umetengeneza breed/ aina ya kuku ambayo haijulikani maana breed huwa zinatengenezwa kitaalamu na kwa utaratibu maalum. Gharama ya kufuga kuku hawa ni kubwa, wanahitaji uangalizi mkubwa na sio wastahimilivu wa magonjwa hivyo ni lazima ufuate utaratibu wa chanjo katika kila hatua zake za ukuaji. Ukifuata taratibu za ufugaji bora utapata faida kubwa sana endapo ukifuga kuku hawa. SIFA ZA KUKU WA KISASA WA MAYAI
➡ Wanataga mayai mengi mpaka mayai 250 – 300 kwa mwaka mmoja
➡ Wanakua haraka
wao wa kutaga mayai ni miaka miwili
➡ Gharama ya kuwatunza ni kubwa kwa sababu wanakula sana kwa hiyo unatakiwa uwe na mtaji mzuri ili kufuga kuku hawa
➡Sio wastahimilivu wa magonjwa licha ya kufugwa ndani
➡ Wanahitaji usimamizi mkubwa sana. - KUKU WA NYAMA (BROILERS)
Hii ni aina ya kuku ambao ni spesho kwa ajili ya nyama.
➡ Kama ilivyo kwa kuku wa kisasa wa mayai hawa pia huzalishwa na makampuni makubwa ya kuzalisha na kuuza vifaranga ambapo huchukua kuku wazazi (parent stock) kutoka nje ya nchi ambao huwatumia kutotolesha vifaranga wa kuku wa nyama. Ni ngumu sana mfugaji kuwa na hiyo stock ya wazazi.
➡ Kuku hawa wanakua kwa muda mfupi sana ambapo ni kati ya wiki nne au sita kutokana na utakavyowatunza ambapo wanakuwa tayari kwa kuuzwa.
➡ Gharama ya kufuga kuku hawa ni kubwa kidogo hivyo unatakiwauwe umeandaa mtaji wa kuku






