WAUME WA AINA HII NI TESO KWA WAKE ZAO
- MNYANYASAJI – Hutafuta ufumbuzi wa matatizo kwa kupiga mke, kutukana matusi na kutoa vitisho.
- MVIVU – Hulala siku nzima, hana mipango yoyote na humtegemea mwanamke kutunza familia.
- MSALITI MBOBEVU – Haheshimu kabisa viapo vya ndoa. Muda wote yeye ni kukimbizana na wanawake.
- MZEMBE – Hatimizi wajibu wake. Hajali watoto, hajali mambo ya familia.
- MTOTO WA MAMA – Mama yake ndio hufanya maamuzi yote kila kitu hadi amuulize mama.
- MWENYE WIVU – Hufuatilia simu ya mke nyendo zake, marafiki zake na haishi kumtuhumu mke.kuwa ana wanaume.
- MRAIBU – Hutawaliwa na uraibu wa pombe, kamari au madawa ya kulevya na tabia hizo zinaharibu nyumba yake
- MWENYE KIBURI – Hata akosee haombi msamaha, anataka mke ndio anyenyekee na kuishi naye kama boss.
- MBAHILI – Pesa anayo lakini amejaa ubinafsi hawezi kutunza familia yake. Utakuta yeye anapendeza ila mke na watoto wanavaa midabwada.
- MSIRI – Yupo kwenye ndoa ila ana maisha yake ya siri. Hamshirikishi mke mipango yake, pesa zake wala maisha yake, anaishi kivyakevyake.
Mwanamke mwenye mume wa aina hii aongeze maombi Mungu bado anaweza. Pia msiache kuhudhuria semina za ndoa zinasaidia sana.






