Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Emmanuel Nchinbi amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itaanzisha mchakato wa mazungumzo ya maridhiano ili kuimarisha umoja, amani na mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza kwa niaba ya Rais, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao Dk. Nchimbi amesema serikali imejizatiti kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuishi kwa utulivu na chini ya misingi ya utawala wa sheria.
“Ni dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunaanzisha mazungumzo ya maridhiano ili hata hao wachache wanapata nafasi ya kusikilizwa na kuwa na taifa lenye amani na utulivu,” amesema Dk Nchimbi akiwashukuru viongozi wa SADC.






