Kaulimbiu yao ni Utumishi kwa Wote. Lakini si polisi wote wanaosadiki maana halisi ya kauli hiyo. Katika siku za hivi majuzi, maafisa wa polisi wamegeuka fisi mla kondoo. Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita pekee, polisi 14 na afisa mmoja wa magereza wamekamatwa kwa makosa mazito yaliyohatarisha maisha ya raia walioapa kuwalinda. Maafisa 10 kati yao wanatuhumiwa kufanya uhalifu mamia ya kilomita kutoka vituo vyao rasmi vya kazi. Source, Taifa Jumapili






