Haiwezekani!
”Hamwezi kusema nyinyi ni Umoja wa Mataifa huku mkiyapuuza mataifa 54 ya Afrika.”
Kauli ya Rais William Ruto akizungumza wakati wa Kongamano la Usalama la Umoja wa Matiafa linaloendelea jijini New York, Marekani.
Rais ameyakosoa mataifa ya magharibi kwa kufanya maamuzi muhimu yakiwamo ya usalama, maendeleo na amani bila kuhusisha Afrika ilhali mataifa ayo hayo yako chini ya mwavuli wa UN -Umoja wa Mataifa.






